AZAM FC WAFUNGA USAJIRI WA MCHEZAJI HUYU

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, imemrejesha kiungo wake mkabaji Stephan Kingue, kwa mkataba wa mwaka mmoja na kufunga usajili wa dirisha dogo unaomalizika leo Jumamosi saa 5.59 usiku.

Kingue aliyekuwa amepumzishwa mara baada ya kupata majeraha kama ilivyokuwa kwa beki kisiki Daniel Amoah, ambaye naye amerejeshwa kwenye usajili wa dirisha dogo, anarejea akiwa fiti kabisa tayari kuendeleza mapambano

LihatTutupKomentar