YANGA YATOA KICHAPO

Na Godfrey Mgaya

Kikosi cha Yanga kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao, 1-0 mbele ya African Lyon katika mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Bao la Yanga lilifungwa na kiungo mshambuliaji Pius Buswita dakika ya 42 kipindi cha kwanza akimalizia pasi ya Yohana Mkomola kwa guu lake la kulia.

 Nahodha msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema bado wana kazi ya kufanya hasa kutokana na kuwa na kikosi ambacho kinazidi kuimarika .

 " Tumecheza na timu imara ndiyo maana ambayo inazidi kutupa nguvu, mchezo  umekuwa na ushindani mkubwa licha ya kuwa wa kirafiki, tumepata matokeo hiyo ni furaha kwetu kwa kuwa bado tunatengeneza timu imara," alisema.

Mshambuliaji wa African Lyon, Ismail Gambo amesema wameshindwa kupata matokeo licha ya  kutengeneza nafasi nyingi ambazo wamezipata.

" Makosa tumeyaona na tutayafanyia kazi kwenye michezo yetu mingine tutakayocheza ili kuweza kupata matokeo kwani tulitengeneza nafasi nyingi," alisema Gambo.

LihatTutupKomentar