YANGA WAMTAKA MCHEZAJI HUYU KUTOKA NDANDA FC



Kuelekea kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili hapa Bongo, unaambiwa klabu ya Yanga tayari imeshaanza mazungumzo na straika wa Ndanda FC, Vitalis Mayanga.

Yanga imeanza kumnyatia mchezaji huyo ambaye amekuwa kwenye fomu ndani ya Ndanda kwa ajili ya kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Mayanga ambaye aliwahi kuichezea Stand United ya Shinyanga anaweza akavaa uzi wa njano na kijani kuanzia tarehe 15 siku ambayo dirisha dogo litafunguliwa.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinaeleza uongozi wa klabu hiyo unaendelea kufuatilia wachezaji wengine kwa siri ambao watatua dirisha dogo ndani ya timu.

Kwa sasa Yanga inaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Bara na mchezo utakaofuata ni dhidi ya Mwadui FC huko Shinyanga.

LihatTutupKomentar