WACHEZAJI WA YANGA WAKACHA MAZOEZI



Mratibu wa timu ya Yanga, Hafidh Saleh ameibuka na kusema kuwa ni kweli jumla ya wachezaji wanne hawakufika mazoezini juzi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini.

Saleh ameeleza kuwa wachezaji walishindwa kufika kutokana na matatizo mbalimbali yaliyowakwamisha na kushindwa kufanya mazoezi.

Wachezaji hao ambao ni Andrew Vincent, Ibrahim Ajibu, Matheo Anthony na Mrisho Ngassa, walishindwa kujumuika katika mazoezi ya juzi na kuzua maswali kwa wanayanga baada ya taarifa zao kuenea.

Saleh amesema mchezaji kama Ajibu bado hajapona vizuri akieleza alikuwa kwenye matibabu huku Matheo aliaga kwenda kwenye msiba wa ndugu yake.

Yanga inaendelea kujifua hivi sasa kujiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Bara ambapo katika mchezo unaofuata itakuwa inakabiliana na Mwadui FC huko Shinyanga.

LihatTutupKomentar