TFF YAFUNGUKA HAYA UCHAGUZI YANGA

Tamko la TFF kuhusu uchaguzi wa Yanga baada ya Manji kurejea

Siku moja baada ya Baraza la wadhamini wa Yanga kusema kuwa Mwenyekiti wao, Yusuph Manji amerejea, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Ally Mchungahela ameibuka na kudai kwamba uchaguzi wa viongozi wa timu hiyo upo pale pale ikiwemo nafasi ya Manji.

Akizungumza na nasi wakili huyo amesema nafasi ya Manji ni miongoni mwa nafasi zinazowaniwa kwenye uchaguzi huo.

“Sisi uchaguzi unaendelea kama kawaida na hata nafasi ya Manji pia watu wanachukua fomu kama tulivyoelekezwa na serikali,” amesema.

Uchaguzi huo umepangwa kufanyika January 13 mwaka huu baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuitaka Yanga kuitisha uchaguzi wake kwa ajili ya kujaza nafasi zilizo wazi ikiwemo ya Manji aliyeandika barua ya kujiuzulu Mei 2017.

LihatTutupKomentar