MECHI ZA VIPORO YANGA KUPIGWA NJE YA DAR



Bodi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) imevipangia tarehe mechi za viporo za Yanga ambazo zote zitachezewa nje ya Dar es Salaam.

Ratiba hiyo inaonesha Yanga itakuwa na kibarua kwenye Uwanja wa CCM Kambarage kucheza dhidi ya Mwadui FC Novemba 22.

AIdha, siku mbili baadaye Yanga itapaswa kuwa mjini Kaitaba, Kagera kukipiga na walima miwa wa mkoani humo, Kagera Sugar.

Viporo hivyo vya Yanga vimetoka na kuchelewa kuanza ligi ambapo timu ilikuwa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

LihatTutupKomentar