SIMBA NA YANGA WAKUTANISHWA NA Mo


Uongozi wa timu ya Simba umesema kuwa hawana ugomvi na timu ya Yanga kwa kuwa wanashirikiana katika masuala muhimu ya maendeleo, ushindani wao upo uwanjani.

Ofisa habari wa timu ya Simba, Haji Manara amesema Yanga ni watu muhimu kwa Simba kwani waliungana nao kufanya dua katika matatizo waliyoyapata hali iliyoleta matokeo mazuri kwa kuwa dua zimejibiwa.

"Yanga ni watu wetu wa karibu hatuna ugomvi nao,wameungana nasi katika kipindi kigumu ambacho tumepitia ,dua zao zimesaidia mpaka kupatikana kwa muwekezaji wa timu yetu Mohamed Dewji "Mo" , hivyo hatuna ugomvi nao"alisema.

LihatTutupKomentar