JOSE MOURINHO AHAMA MAKAZI KISA MASHABIKI


Kutokana na timu yake kufanya vibaya katika Ligi Kuu England, Kocha wa Manchester United amezidi kuwashangaza wengi kwa kuendelea kukaa hotelini.

Mourinho ambaye ameingia kwenye tetesi kubwa za kufukuzwa kazi kutokana na aina ya mpira ambao United inacheza na matokeo, imeelezwa mpaka sasa hajachukua nyumba katika mji wa Manchester.

Maamuzi hayo ya Mourinho yanaelezwa kutokana na kujawa na hofu juu ya hatma yake na United akiamini muda wowote anaweza akaondoshwa.

Kocha huyo aliepuka kufukuzwa kibaruani kufuatia kupata ushindi wa mabao wa mbinde 3-2 dhidi ya Newcastle United kwenye Uwanja wa Old Trafford.

LihatTutupKomentar