WAKALA WA MBWANA SAMATTA AFUNGUKA HAYA


Baada ya kuzuka tetesi jana juu ya Mtanzania, Mbwana Samatta anayekipiga katika klabu ya KRC Genk huko Ulaya, wakala wa mchezaji huyo, Jamali Kisongo, ameibuka na kukanusha habari hizo.

Iliripotiwa kuwa Samatta ameanza kuwindwa na timu kadhaa zinazoshiriki Ligi Kuu England ikiwemo Everton, Brighton, West Ham na Aston Villa.

Kisongo amesema kuwa hizo ni tetesi tu ambazo zimezushwa na hazina ukweli wowote juu ya mchezaji wake kuelekea huko.

Aidha, Kisongo amesema hakuna haja ya kuzidi kuzisambaza zaidi kwani zinaweza zikamuathiri Samatta ambaye nguvu zake zote hivi sasa ziko ndani ya klabu yake.

Mshambuliaji huyo tegemo ndani ya timu hiyo amesafiri na kikosi cha Stars usiku wa kuamkia leo tayari kwa mchezo dhidi ya Cape Verde utakaopigwa Oktoba 12 2018.

LihatTutupKomentar