AL AHLY VS ETOILE DU SAHEL KUKUTANA FINALI

FAINALI ya Ligi ya Mabingwa Afrika itazikutanisha timu za Kaskazini mwa Afrika tupu, Al Ahly ya Misri na Etoile du Sahel ya Tunisia.
Hiyo ni baada ya vigogo hao wa Kaskazini mwa Afrika kuwatoa wapinzani wao katika hatua ya Nusu Fainali kufuatia mechi za marudiano jana.  
Etoile du Sahel iliibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Primiero de Agosto ya Angola usiku wa jana Uwanja wa Olimpiki mjini Rades na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-3.
Hiyo ni baada ya kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza  Uwanja wa Novemba 11 mjini Luanda Oktoba 2 mwaka huu, bao pekee la kiungo Luvumbo Pedro ‘Bua’ dakika ya 80.


Na jana mabao ya Etoile yalifungwa na mshambuliaji Mualgeria Mohamed Youcef Belaili kwa penalti dakika ya 16, Watunisia beki Mohamed Ali Yacoubi dakika ya 27, washambuliaji Haythem Jouini dakika ya 73 na Anice Badri dakika ya 85, wakati ya Primiero de Agosto yalifungwa na Hermenegildo Costa Paulo Bartolomeu ‘Geraldo’ dakika ya nane na Mkongo Mongo Kipe Lumpala Bokamba dakika ya 64.
Nayo ES Setif ikaichapa Al Ahly mabao 2-1 katika mchezo mwingine wa marudiano hatua ya Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Mei 8, 1945 mjin Setif.
Lakini pamoja na ushindi huo, safari ya Setif inaishia hapa baada ya kufungwa 2-0 kwenye mechi ya kwanza Oktoba 2 Uwanja wa Al Salam mjini Cairo, mabao ya Walid Soliman dakika ya 23 na Islam Mohareb dakika ya 41 na sasa wanatolewa kwa jumla ya mabao 3-2.  
Jana mabao ya Setif yalifungwa na  Mohamed Islam Bakir dakika ya 67 na Houssam Eddine Ghacha dakika ya 72, baada ya Walid Soliman kutangulia kuifungia Al Ahly dakika ya 61.
Nusu Fainali ya kwanza itachezwa Novemba 2 nchini Misri kabla ya timu hizo kurudiana Novemba 9 nchini Algeria. 
Ikumbukwe, Setif ndiyo iliyowatoa waliokuwa mabingwa mtetezi, Wydad Casablanca ya Morocco katika hatua ya Robo Fainali ikiwachapa 1-0 Algeria kabla ya kwenda kutoka nao sare ya 0-0 Casablanca.

LihatTutupKomentar