TETESI ZA USAJIRI ULAYA LEO

Kiungo wa kati wa Chelsea raia wa Brazil Willian, 30, anasema hakuwa na mpango wa kuondoka stamford Bridge msimu huu licha ya vilabu vya Manchester United na Barcelona kuonyesha dalili ya kumsaini. (Express)

Mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 20, anapata mafunzo zaidi kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Manchester United Romelu Lukaku.
Meneja wa England Gareth Southgate amemtuma naibu wake Steve Holland kumtazama Jack Grealish wakati wa ushindi wa Aston Villa dhidi ya Rotherham siku ya Jumanne wakati anafikiria kumsaini kiungo huyo wa kati wa umri wa miaka 23. (Birmingham Mail)

Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 33, anasema itakuwa vigumu kwa mtoto wake wa umri wa miaka nane ambaye pia anaitwa Cristiano kucheza mpira kama yeye. Ronaldo Junior anaichezea Juventus Academy. (BeIn Sports, via Sun)
Totttenham wametupilia mbali madai kuwa uwanja wao mpya hautakuwa tayari ifakapo mwanzo wa mwaka 2019. (Sky Sports)
Wachezaji wanaoongoza ufungaji wa mabao ligini England
Mkuu mpya wa kandanda huko Arsenal Raul Sanllehi, anataka kumsaini wing'a raia wa Argentina Cristian Pavon, 22, kutoka Boca Juniors. (Football London)
Beki wa Manchester City Aymeric Laporte, 24, anasema ataendelea kuwepo kuichezea Ufaransa licha ya ripoti kuwa huenda anageuza uzalendo wake kwa Uhisania. (Manchester Evening News)
Mshambualiaji wa Liverpool Sadio Mane, 26, amemshauri Roberto Firmino kucheza dhidi ya Paris St-Germain licha ya jeraha lake la jicho.
Mshambuliaji huyo wa Brazil ambaye pia ana miaka 26 alitoka nje na kufunga bao la ushindi siku ya Jumanne. (Liverpool Echo)

Kiungo wa kati wa England James Milner, 32, anasema alipigwa marufuku ya kuvaa nguo nyekundu akiwa mtoto kwa sababu baba yake alikuwa anaichukia Manchester United. (FourFourTwo)
Kipa wa Arsenal Petr Cech, 36, anacheza kupata hatma yake kwa Gunners wakati yuko katika mwaka wake wa mwisho wa mkataba huku akikabiliwa na ushindani kutoka kwa Mjerumania Bernd Leno, 26. (Evening Standard)
Mtoto wa wing'a wa zamani wa Manchester City, QPR na England Shaun Wright-Phillips, 36, alifanya mazoezi na kikosi cha kwanza kablka ya mechi yao na Lyon. D'Margio Wright-Phillips, 16, pia yeye ni wing'a na anachezea kikosi cha City chini ya miaka 18. (Mail)
Bora Kutoka Jumatano
Manchester City bado hawajaanza mazungumzo ya mkataba na wing'a mwenye miaka 23 Raheem Sterling, lakini sasa wanataka kufanya mazungumzo kuhusu kuongeza mkataba huo ambao utakamilika mwaka 2020. (Sun)
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ametajwa k amamtu anayeweza kuwa mwenyekiti wa siku za usoni wa shirika linalosimamia Ligi ya Premia. Hilo lilifanyika wakati wa mazungumzo ya hivi karibuni ya klabu za England. (Daily Mail)
Brighton wanataka kumteua mkurugenzi wa kiufudi wa FA Dan Ashworth katika nafasi sawa na hiyo kwenye klabu yao.
Mlinzi wa Leicester raia wa England mwenye miaka 25 Harry Maguire amekana ripoti kuwa wachezaji hawakufurahishwa baada ya wao kusafiri kwa magari badala ya ndege kwa mechi huko Bournemputh. (Leicester Mercury)
Afisa mmoja wa West Brom aliondoka klabu hiyo baada ya uamuzi wa kukosa kununuliwa Virgine van Dijk kutoka Celtic licha ya kumpendekeza. (Scottish Sun)
Ajenti wa Mesut Ozil amewakashifu Manuel Neuer, Thomas Muller na Toni Kroos kufuatia matamshi waliyotoa baada ya uamuzi wa kiungo huyo wa kati wa Arsenal wa kuacha kuichezea Ujerumani mechi za kimataifa. (Guardian)
Meneja wa England Gareth Southgate alienda kutazama mechi ya nyumbani kati ya Derby na Blackburn Rovers badala ya mechi la ligi ya mabigwa kati ya Liverpool na Paris St-Germain siku ya Jumanne. (Times)

LihatTutupKomentar