SIMBA WANAENDELEA KUNOA SIRAHA ZAO

Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi jioni ya leo Jumatano katika Uwanja wa Boko Veterans uliopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Simba wameanza na mazoezi ya nguvu kwa kila mchezaji kufanya ambayo amepangiwa na kocha wa viungo Adel Zrane.
Katika mazoezi hayo yalikuwa katika makundi tofauti. Kuna ambao walibeba chuku, kuvuta kamba, kuruka viunzi na mengine mengi.
Dhumuni la mazoezi haya ya kuwepo kwa vifaa vingi vya kufanyia mazoezi ni kuongeza utimamu wa mnwili kwa wachezaji wa kikosi hiko.
Huenda kocha wa Simba Patrick Aussems akawa anawafanyisha mazoezi hayo kutokana na mapungufu ya wapinzani wao Yanga.
Aussems amezungumza na Mwanaspoti kwamba wapinzani wao Yanga mwanzo wa mchezo wanakuwa vizuri lakini kadri muda unavyozidi kwenda wanapoteza spidi walioanza nayo.

LihatTutupKomentar