RATIBA LIGI KUU TANZANIA BARA YAPANGULIWA TENA


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limeahirisha mechi za Simba dhidi ya Biashara United pamoja na Yanga dhidi ya JKT Tanzania Tanzania.

Yanga ilitakiwa kukipiga na JKT Septemba 26 2018 wakati Simba ikipaswa kucheza na Biashara Septemba 27 mechi zote zikafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, sasa zitapangiwa tarehe nyingine.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya uongozi wa Simba kutuma maombi ya kuomba mechi yao na Biashara United isogezwe mbele ili kuwapa nafasi ya kujiandaa na mechi dhidi ya Yanga.

Kwa mujibu wa Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah, alieleza wameamua kuomba mechi na Biashara iahirishwe ili wapate muda mzuri kujiwinda na Yanga kwa maana ratiba itakuwa inawabana.

Baada ya maombi hayo kufika TFF, imeelezwa taayari wameridhia maombi hayo na sasa mechi hiyo itapangiwa tarehe nyingine pamoja na ile ya Yanga dhidi ya JKT Tanzania.

LihatTutupKomentar