KUELEKEA MCHEZO WA WATANI WA JADI SIMBA VS YANGA SIMBA ITAWAKOSA HAWA HAPA




Kuelekea mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga itakayopigwa Septemba 30 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wekundu wa Msimbazi wako kwenye hatihati ya kuwakosa wachezaji wawili.

Mzamiru Yassin na Hassan Dilunga ndiyo wachezaji ambao hawako fiti kiafya mpaka sasa kutokana na kuwa majeruhi, jambo ambalo lilipelekea wasifanye mazoezi jana.

Katika mazoezi ya jana yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Yassin na Dilunga hawakuweza kuwa sehemu ya kikosi, na hii ni juu ya afya zao kutokuwa sawa.

Mbali na wawili hao, kuelekea mechi hiyo yenye msisimko wa aina yake, Simba itamkosa pia Nahodha wake, John Bocco ambaye atakuwa anatumikia adhabu ya kuwa na kadi nyekundu.

Bocco alipata kadi hiyo katika mchezo na Mwadui FC uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Mwadui wakati pambano likiendelea.

LihatTutupKomentar