KINACHO ENDELEA SIMBA NA KOCHA MASOUD DJUMA HIKI HAPA

Moja kati ya taarifa zinazozidisha tetesi kubwa katika mitandao ya kijamii katika soka la Bongo ni hii ya kocha msaidizi wa Simba SC raia wa Burundi Masoud Djuma kudaiwa kuwa ataachwa Dar es Salaam wakati timu ikisafiri kwenda Mwanza.
Simba weekend iliyomalizika ilicheza game yake ya Ligi Kuu Mtwara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona na kulazimishwa sare tasa dhidi ya Ndanda FC lakini benchi akikosekana kocha msaidizi wa timu hiyo Masoud Djuma akiwakasalia Dar es Salaam.
Maswali yamezidi kuwa mengi baada ya September 17 kuripotiwa kwa taarifa kuwa Masoud Djuma, anaweza akaachwa tena Simba ikielekea Mwanza kwa ajili ya game zake za Kanda ya Ziwa za Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2018/19 kati ya Mbao FC na Mwadui.
Simba ambao wanaripotiwa kuwa watasafiri leo, kwa mujibu wa muandishi wa habari za michezo wa Champions Saleh Jembe, ameripotiwa Masoud Djuma kuna uwezekano mkubwa wa kutokuwa sehemu ya timu tena kama ilivyokuwa katika safari ya Mtwara na atabaki Dar es Salaam, bado haijaeleweka kuna nini kinaendelea japo watu wanadai kuwa kocha mkuu na Masoud Djuma inawezekana wakawa wamepishana kauli.
LihatTutupKomentar