JKU YAWEWESEKA NA UBINGWA

KOCHA wa timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar JKU inayoshiriki ligi kuu ya Zanzibar hatua ya nane bora Hassan Ramadhan, amesema matarajio yao kuchukua ubingwa kwa mara ya pili ili kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.
Akizungumza na gazeti hili alisema kikosi chake kinaendelea kupambana na imani yao watafanikiwa kutwaa ubingwa huo.
Alisema wachezaji wamekuwa na bidii na hamu kubwa ya kutwaa taji hilo kwa kufanya mazoezi, na kusikiliza maelekezo wanayopewa na walimu wao wakiwa uwanjani.
Hata hivyo alisema wapo wachezaji wawili majeruhi na wanaendelea vyema hata hivyo amejinasibu kuwa, haitoathiri kitu kwani watapambana hadi mwisho.
Aidha alisema umoja na mshikamano wa viongozi na wachezaji utaifanya timu yao kufanya vyema katika mchezo uliosalia.
Hassan alieleza kuwa wamecheza mechi 12, na wana pointi 27 huku wakishinda michezo minane,wametoka sare michezo mitatu na kufungwa mchezo mmoja.
Alitoa wito kwa wadau wa timu hiyo kuendelea kuwaunga mkono ili kupata nguvu ya pamoja kwa ajili ya kufanya vyema na kutimiza malengo yao.
LihatTutupKomentar