HISTORIA YA WATANI WA JADI SIMBA VS YANGA KWA MIAKA KUMI

Na
Godfrey Mgaya
Hayawi hayawi yamekuwa. Lile pambano la watani wa jadi Yanga na Simba lililosubiliwa kwa wiki kadhaa sasa limefika litachezwa juma pili saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Katika kuelekea mchezo huo, mkomesportnews nakuletea takwimu za miaka 10 iliyopita kuanzia Julai 8, 2007 hadi leo.

Julai 8, 2007
Simba na Yanga ziliumana katika mchezo wa fainali ya nane bora uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro ambapo zilimaliza dakika 120 kwa sare ya bao 1-1. Bao la Simba lilifungwa na Moses Odhiambo dakika ya 2 na Said Maulid alisawazisha dakika ya 55. Simba ilishinda kwa penati 5-4.

Oktoba 24, 2007
Simba iliendeleza ubabe kwa Yanga kwa kuichapa bao 1-0 lililofungwa na winga hatari, Ulimboka Mwakingwe. Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri.

April 27, 2008
Miamba hiyo ya soka nchini ilitoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa jijini Dar es Salaam.

Oktoba 26, 2008
Yanga ikisheheni mastaa lukuki wakiwemo Bernad Siange Mwalala, Boniface Ambani, George Owino, Geofrey Bonny na Mrisho Ngassa iliitandika Simba bao 1-0 lililofungwa na Mwalala dakika ya 15 baada ya kupokea pasi ya Ambani. Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Taifa.

April 19, 2009
Yanga na Simba zilifungana mabao 2-2 katika mchezo uliokuwa na ushindani mkali baina ya timu hizo. Simba ilipata mabao yake kupitia Ramadhan Chombo dakika ya 23 na Haruna Moshi dakika ya 62 wakati Yanga ilisawazisha kupitia Ben Mwalala dakika ya 48 na Jerry Tegete dakika ya 90.

Oktoba 31, 2009
Mussa Hassan ‘Mgosi’alifunga bao pekee dakika ya 26 lililoipa Simba ushindi wa bao 1-0.

April 18, 2010
Mgosi alirudia tena kuisumbua Simba ambapo alifunga mabao mawili na kuiongoza Simba kuishinda Yanga kwa mabao 4-3. Mgosi alifunga mabao yake dakika za 53 na 74. Mabao mengine ya Simba yalifungwa na Uhuru Seleman dakika ya 3 na Hillary Echesa dakika ya 90. Mbao ya Yanga kwenye mechi hiyo yalifungwa na Jerry Tegete dakika ya 69 na 89 na bao jingine lilifungwa na Athuman Idd dakika ya 30.

Oktoba16, 2010:
Pambano la watani wa jadi lilipigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo Yanga iliikung’uta Simba bao 1-0 lililofungwa na Jerry Tegete dakika ya 70

Machi 5, 2011
Timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 ambapo bao la Yanga lilifungwa na beki Stephano Mwasika kwa penati dakika ya 59 na Simba ilisawazisha dakika ya 73 kupitia Mussa Hassan Mgosi. Katika mchezo huo, mwamuzi Orden Mbaga alizua kashikashi uwanjani baada ya kulikataa bao la kusawazisha la Simba kasha kulikubali baada ya kujadiliana na msaidizi wake namba moja.
(Refa Orden Mbaga alizua tafrani uwanjani, kwanza kwa kulikataa bao la kusawazisha la Simba, kisha akalikubali baada ya kujadiliana na msaidia wake namba moja).

Oktoba 29, 2011
Yanga iliibanjua Simba bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji raia wa Zambia Davies Mwape dakika ya 75 ya mchezo.

Mei 6, 2012
Simba ikiwa chini ya Kocha Milovan Cirkovic ilipata ushindi mkubwa dhidi ya Yanga tangu kuanza kwa karne ya 21 kwa kuinyuka mabao 5-0. Katika mchezo huo ambao Yanga ilizidiwa tangu mwanzo mabao ya Simba yalifungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 1 na 65, Felix Sunzu dakika ya 74, Pastrick Mafisango dakika ya 58 na Juma Kaseja aliyefunga dakika ya 69.

Oktoba 3, 2012
Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 ambao Simba ilitangulia kufunga kupitia Amry Kiemba ‘Father’ dakika ya 3 na Yanga ilifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 64 kwa njia ya penati baada ya beki Paulo Ngalema kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Oktoba 20, 2013
Matokeo ya maajabu katika pambano la watani wa jadi. Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-0 lakini Simba ilirudi na kufanikiwa kurudisha mabao yote na kufanya mchezo umalizike kwa sare ya mabao 3-3. Mbao ya Yanga yalifungwa na Hamis Kiiza aliyefunga mawili na Mrisho Ngassa wakati Simba ilisawazisha kupitia Joseph Owino, Betram Mwombeki na Gilbert Kaze.

Aprili 20, 2014
Simba na Yanga zilitoka suluhu katika mchezo ambao Yanga ilitawala kwa asilimia kubwa. Mchezo huo uligharisha nyota ya kipa chipukizi Manyika Peter ambaye ndio jkwanza alikuwa amepandishwa kwenye kikosi cha wakubwa cha Simba.

Machi 8, 2015
Simba iliitandika Yanga bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Emanuel Okwi likiwa ni bao lake la tatu kwenye mechi za Ligi Kuu zilizoikutanisha miamba hiyo ya soka.

Oktoba 20, 2015
Mshambuliaji Amiss Tambwe ambaye awali alikuwa Simba aliijerehi klabu yake ya zamani na kuingoza Yanga kushinda mabao 2-0. Bao lingine la Yanga lilifungwa na Malimi Busungu.
Februari 20, 2016
Yanga iliendeleza ubabe kwa Simba huku mshambuliaji Amiss Tambwe akiijerehi kwa mara ya pili klabu yake ya zamani. Yanga ikiwa na kikosi bora kilichowahusisha Donald Ngoma, Kelvin Yondan, Deus Kaseke, Simon Msuva na wengineo iliizaba Simba mabao 2-0 ambapo mbali na Tambwe goli lingine lilifungwa na Donald Ngoma aliyezawadiwa pasi Hassan Kessy.

Oktoba 1, 2016
Pambano la watani lililokuwa na tafrani baada ya mwamuzi Martin Sanya kulikubali bao la ‘mkono’ la Amiss Tambwe na kuzusha ghasia baada ya mashabiki wa Simba kung’ao viti na kuvitupa uwanjani. Simba ilikomboa bao hilo dakika ya 87 kupitia kona ya Shiza Kichuya iliyokwenda moja kwa moja kimiani.

Februari 25, 2017
Pambano la mzunguko wa pili wa Ligi Kuu lilimalizika kwa Simba kushinda mabao 2-1 yaliyofungwa na Laudi Mavugo dakika ya 66 na Shiza Kichuya dakika ya 81. Bao la kufutia machozi la Yanga lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Simon Msuva dakika ya 5 baada ya beki Naovalty Lufunga kumwangusha Obrey Chirwa kwenye eneo la hatari.

October 28, 2017
ilichezwa mechi ya ligi kuu Tanzania bara ‘Dar derby’ Yanga vs Simba imechezwa kwenye uwanja wa Uhuru na timu hizo kutoka sare ya kufungana 1-1.
Simba walitangulia kupata goli kupitia kwa kiungo wao mshambuliaji Shiza Kichuya dakika ya 58 kipindi cha kwanza, Yanga wakasawazisha dakika mbili baadae goli likifungwa na Obrey Chirwa.

April 29,2018
Pambano la watani wa jadi lililo kutanisha wababe hao wote wakiwa fiti ambapo SIMBA walipata usindi wa bao 1-0 lililo fungwa na Erasto Nyoni
Ka hapa hapa tutaendelea kukujuza zaidi

LihatTutupKomentar