GABO ALIA JAMII KUPENDA UMBEYA

MWIGIZAJI bora wa kiume nchini, Salim Ahmed ‘Gabo’, amesema umefika muda wa jamii kutumia muda mwingi katika mambo ya maana na kuacha kushabikia matukio ya umbea ambayo hayana faida.

Gabo, ameliambia Papaso la Burudani kuwa anaamini kuna watu wanafanya mambo mengi ya msingi lakini hawapati nafasi kubwa kama wanayopata wale wanaotenda matendo machafu katika jamii jambo ambalo halipendezi.

“Binafsi nimefanya mambo mengi mazuri na makubwa yenye manufaa katika Taifa letu, lakini hayapati nafasi kwenye jamii kama yanavyopata mambo mengine ya umbea na ya mtu binafsi yasiyo na faida, hii inaonyesha wazi kuwa Watanzania wengi wanapenda kufuatilia vitu visivyokuwa na faida kwao,” alisema Gabo.

LihatTutupKomentar