BOSI YANGA AMWAGA DONGE NONO JANGWANI

Kiongozi wa Yanga Morogoro, Hamad Islam juzi Ijumaa alivamia mazoezi ya Yanga na kutoa ahadi kwa kocha wa timu hiyo, Mcongo, Mwinyi Zahera.

Yanga ambayo iliweka kambi mkoani Morogoro tangu Jumatatu ya wiki hii na juzi Ijumaa ilitarajiwa kurejea jijini Dar tayari kwa mchezo wao dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar leo Jumapili.

Gazeti la Championi ambalo lilikuwepo uwanjani hapo, lilimshuhudia kiongozi huyo baada ya mazoezi kumalizika akiwa na Yondani na kumuuliza wao kama wachezaji wangependa kufanyiwa nini baada ya mechi.

Baada ya swali hilo, Yondani alimjibu kuwa kama kutakuwa na bonasi waambiwe ni kiasi gani ili wachezaji wawe na taarifa kuwa watapewa kiasi gani kama wakishinda mchezo huo.

Hata hivyo bosi huyo, alisema angekwenda kuzungumza kwanza na wenzake wa kamati ya utendaji watakaokutana leo Jumamosi kujadili kiasi ambacho watawapa wachezaji wao.

Aidha Islam aliliambia Championi Jumamosi kuwa, amepanga kumpa dola 200 Kocha Zahera ambazo ni Sh 456,306 ikiwa tu timu itapata ushindi wowote. 

“Nimepanga kumpa dola 200 kocha kama timu itashinda,” alisema Islam.

LihatTutupKomentar