WAKALA WA POGBA AWEKA NGUMU


Ajenti wa mcheza soka wa Manchester United, Mino Raiola, anafanya juhudi za kumwondoa mchezaji huyo katika timu hiyo ya Uingereza ili aende kuchezea timu ya Barcelona. 

Raiola amekuwa akifanya juhudi hizo kwa muda wa miaka miwili tangu Pogba alipohama timu ya Juventus na kujiunga na United kwa Paundi mil. 89 (Sh. bil. 263). 

Mchezaji huyo hivi sasa amerejea Uingereza akitokea kwao Ufaransa baada ya kutwaa Kombe la Dunia  nchini Urusi. 

Hata hivyo, United wamesisitiza jana (Jumatatu) kwamba hawamuuzi mchezaji huyo na wamekataa ofa ya Barcelona ya Paundi mil. 44.6 (Sh. bilioni 132) na kupewa pia wachezaji  Yerry Mina na Andre Gomes. 

Kwa vile msimu wa ligi kuu unaanza Ijumaa wiki hii kwa United kucheza nyumbani dhidi ya Leicester, huenda mpango huo ukafanyika wakati wa dirisha dogo.

I

LihatTutupKomentar