MOHAMED MWAMEJA NO, ESSAM EL- HEDDARY YES.

Essam El- Heddary ametangaza kuachana na soka la kimataifa. Amestaafu. Ni golikipa ambaye ameniacha na maswali mengi ya kujiuliza. Ni maswali ambayo sina majibu ya haraka haraka ambayo ninaweza nikajibu. Umri wa Essam El- Heddary ni mkubwa kuliko wachezaji wote ambao walishiriki michuano ya kombe la dunia pale Russia. Ana umri wa miaka 45. Essam El- Heddary ametwaa kila kitu ndani ya ardhi ya Afrika. Ametwaa kombe la Afcon mara 4 akiwa na timu ya taifa ya Egypt. Ametwaa kombe la klabu bingwa na kombe la shirikisho barani Afrika akiwa na vilabu tofauti tofauti pale Egypt. Essam El- Heddary hatumdai.

Mwaka 1993 wakati Simba wakicheza fainali ya kombe la shirikisho na klabu ya Stella Abdjan golini alikuwepo Mohamed Mwameja. Ni miongoni mwa magolikipa bora ambo wamewahi kutokea nchini Tanzania. Akiwa na Simba Mwameja hakuwahi kupata mafanikio mengine zaidi makubwa zaidi ya kucheza fainali hizo za mwaka 1993. Mafanikio mengine ni kutwaa kombe la ligi kuu ambalo hata Manula Aishi ametwaa .Mwaka 1996 yaani  miaka mitatu baadae Mwameja alienda zake Reading pale England. Hakuna maajabu yeyote ambayo Mwameja aliyafanya akiwa na Reading. Hii ni kwa mujibu wa wikipedia. Mwaka 1998 Mwameja alirudi Simba na 

na mwaka 2001 Mwameja akatangaza kuachana na soka. Habari ya Mwameja ikawa imeishia hapo. Kuanzia hapo Tanzania tukaendelea kuwa na idadi finyu ya magolikipa ambao wanacheza soka nje ya nchi. Sina uhakika sana kama Idd Pazi "Father" aliwahi kucheza soka la kulipwa nje ya nchi. Sina uhakika. Kuna tatizo moja ambalo linaleta tofauti kati ya Mohamed Mwameja na Essam El Heddary. Ligi kuu ya Egypt inaendeshwa katika misingi ya weledi kwa miaka nenda rudi. Timu shiriki za ligi kuu ya Egypt zinalipa mishahara mikubwa wachezaji wao. Mishahara na posho ambazo baadhi ya wachezaji hawalipwi. Hii ndiyo sababu ambayo

ilimpa kiburi Essam El Heddary pale Egypt. Mohamed Mwameja sidhani kama ana utajiri unaokaribiana hata robo tu na utajiri wa Essam El- Heddary. Ligi yetu kwa muda mrefu ilikuwa inaendeshwa pasipo kufuata misingi ya weledi. Huenda wakina Mohamed Mwameja au Idd Pazi enzi zao walikuwa wanacheza soka kama kufurahisha mashabiki pamoja na viongozi wa timu zao. Ilikuwa ni kipindi hicho. Sasa hivi ni kosa kubwa kufanya hivyo. Sasa hivi mpira ni biashara kama zilivyo biashara nyingine. Ni ngumu kwa sasa kumsajili mchezaji kwa kumpa saa ya ukutani. Usiwaone wa kina Ivo Mapunda au Deogradius Munishi wanaenda    

kucheza soka nje ya nchi. Wanajua soka ni ajira ambayo inawafanya walee familia zao, wasomeshe wadogo zao, nk. Mohamed Mwameja sina ujasiri wa kusimama mbele na kumtetea kwa kumlinganisha na Essam El- Heddary ambaye amestaafu masaa 48 yaliyopita. Huwa zinafika nyakati katika maisha unapaswa uwe mvumilivu tu. Mohamed Mwameja hakuonekana kuwa na ujasiri huo pale England. Leo hii huenda angekuwa ni mchezaji mstaafu ambaye ni tajiri. Sitaki kujua sana watu waliokuwa wanaomsimamia kwa maana ya kumshauri kusaini mikataba ya ajira pamoja na matangazo. Lakini twende mbele turudi nyuma kura yangu nampa farao.

LihatTutupKomentar