SIRI YA MAFANIKIO YA TIMU YA UFARANSA HAYA HAPA.

Na
 MOSES FRANCIS+255715878724
Baada ya kuisha kwa vita ya pili ya dunia mwaka 1945 nchini nyingi barani Ulaya ziliathirika kiuchumi. Miongoni mwa nchi hizo ilikuwa ni nchi ya Ufaransa ambayo uchumi wake ulikuwa umeharibiwa na vita ya pili ya dunia. Kwahiyo serikali ya nchi ya Ufaransa iliamua kubeba jukumu la kuufufua uchumi wa nchi hiyo. Miongoni mwa njia iliyotumika kuujenga uchumi wa nchi ya Ufaransa ilikuwa ni kuajiri wafanyakazi mbalimbali kutoka kusini na mashariki mwa bara la Ulaya pamoja na kasikazini mwa bara la Afrika hasa katika nchi ya Algeria. Wafanyakazi hawa walienda nchini Ufaransa kwa lengo la kwenda kufanya kazi kwa
dhumuni la kuongeza uzalishaji ambao ulikuwa umeshuka katika nchi hiyo. Mpaka kufikia mwaka 1950 nchi ya Ufaransa ilikuwa ndiyo nchi ambayo ina idadi kubwa ya raia ambao ni wahamiaji ambao walikuwa milioni 2 .7 ikifuatiwa na nchi ya Ujerumani ambayo ilikuwa na wananchi wahamiaji wapatao milioni 2.3. Ilipofika miaka ya 1960 uchumi wa nchi ya Ufaransa ulikuwa tayari umeimarika. Serikali ya nchi ya Ufaransa ilikuwa imefanikiwa kuufufua uchumi wa nchi hiyo, lakini kuna tatizo moja ambalo lilikuwa linaikabili nchi hiyo. Lilikuwa ni tatizo la uhaba wa wafanyakazi (labour shortage). Wafanyakazi walikuwa 
hawatoshi hasa katika mashirika au makampuni yaliyokuwa yanamilikiwa na serikali. Kwahiyo serikali ya nchi ya Ufaransa ikaendelea tena kutafuta wafanyakazi kutoka nje na nchi ya Ufaransa. Wafanyakazi hawa wengi wao walitoka katika nchi za kiarabu pamoja na katika makoloni ya Ufaransa kutoka barani Afrika ambayo yalijulikana kama  (Second French Colonial Empire) . Wakati huo huo nchi ya Ufaransa ilikuwa haifanyi vizuri katika michezo hasa katika mpira wa miguu yaani Football. Timu ya taifa ya Ufaransa ilishindwa kufuzu katika michuano ya kombe la dunia ya mwaka 1962, 1970, 1974. Lilikuwa ni anguko baya la kisoka katika nchi ya Ufaransa. Shirikisho la soka la nchini Ufaransa (FFF) likaamua kuja na mkakati wa koboresha soka katika nchi hiyo. Miongoni mwa mikakati ambayo ilifanywa na shirikisho hilo ni pamoja na kujenga vituo vya mpira wa miguu vya watoto wadogo nchi nzima yaani (Youth Soccer Sports Academies). Ujenzi wa miundombinu hii ya soka ulianza mwaka 1972 na miongoni mwa kituo bora cha kulelea vipaji vya soka nchini humo kinaitwa BIENVENUE A CLAIREFONTAINE ambacho kilijengwa nyakati hizo. Matunda ya uwekezaji katika soka la Ufaransa yalianza kujitokeza katika fainali za kombe la dunia 1998
zilizofanyika nchini humo, ambapo timu ya taifa ya Ufaransa ilinyakua taji hilo la dunia, huku ikiwa na kizazi cha dhahabu chenye asili tofauti tofauti ambapo asili yake nimeizungumzia hapo mwanzo. Mfano kikosi cha Ufaransa cha mwaka 1998 kilichotwaa kombe la dunia kiliundwa na wachezaji kama Zinedine Zidane, Patrick Vieira, Marcel Dessailly, Emmanuel Petit, Fabian Barthez na wengineo wengi. Baada ya kuwa imepita miaka 20 timu ya taifa ya Ufaransa inafanikiwa tena kutwaa kombe la dunia. Imetwaa kombe la dunia nchini Russia mwaka huu huku kikosi cha Ufaransa kikiwa na rundo la wachezaji wenye asili 
na Afrika pamoja na mataifa mengine. Leo hii timu ya taifa ya Ufaransa ina Kliane Mbappe ambaye ana asili ya Afrika kwani wazazi wake wote ni waafrika baba yake anatoka nchini Cameroon na mama yake anatoka nchini Algeria. Kwahiyo tunapozungumzia mafanikio ya timu ya taifa ya Ufaransa yanajengwa na uti wa mgongo ya kutumia wachezaji wenye asili tofauti tofauti. Hawa kina Paulo Pogba, Ngolo Kante, Blaise Matuidi, Mousa Dembele, Steven Mandanda, Steven Nzonzi, na wengineo wamezaliwa Ufaransa lakini wazazi wao walifika Ufaransa kama vibarua.

LihatTutupKomentar