SIMBA INGEANZA NA SAID JUMA MAKAPU.

Na  MOSES FRANCIS
+255715878724
Juma Said Makapu ndiye beki pekee mtanzania mwenye umbo la mvuto. Umbo lake ni hazina tosha. Soka la kisasa linahitaji wachezaji wenye kiimo kirefu na maumbo makubwa. Makapu huwa napenda sana kumfuatilia. Huwa ananivutia. Anajua kucheza mipira ya juu. Anajua kukaba. Yondan Kelvin umri umesogea pia ana kimo kifupi. Katika mpira wa sasa ni ngumu kwa timu za Ulaya kuulizia bei ya Yondan lakini ni rahisi kuulizia bei ya Makapu. Najiuliza kwanini Simba hawajaenda kwa Makapu wameenda kwa Wawa Paschal. Wawa umri umesogea. Makapu umri bado. Lilikuwa ni jambo la kumpa muda na kumwamini tu. Kuna tatizo mahala
Ifike wakati watu wanaotafuta vipaji nchini wawe na jicho la tatu pindi wanapotafuta wachezaji. Watimize majukumu yao ipasavyo. Tanzania ina rundo la vijana wenye vipaji na maumbo makubwa kama ya kina Paschal Wawa au Yakubu Mohamed. Ni vijana ambao huwa wana kufa na vipaji vyao na kubaki tunahaha kutafuta wachezaji wa nje. Kuna wachezaji wenye umri na umbo kama la Juma Makapu ambao wapo nje na Tanzania ambao ni ngumu kuja kucheza ligi ya Tanzania. Mawakala wao kila siku wanapigiwa simu kutoka Afrika Kusini, Morocco, Egypt,  au Ubelgiji. Ligi yetu imejaa wachezaji wa kigeni ambao walio wengi ni wazee.  Hawa ndio kina Paschal Wawa ambaye nasikiasikia kabla hajaja Simba alikuwa hana timu. Wawa hawezi akacheza timu kubwa ligi kuu ya Morocco au Kongo. Ni Tanzania tu ambapo timu zetu za Simba na Yanga zina watu ambao ni wavivu wa kutafuta vipaji ndani na nje ya nchi. Ifike wakati tutambue soka la kisasa  jinsi linavyoendeshwa. Simba mwakani kwenye mechi za kimataifa ingeweza kuwasimamisha mabeki wake wawili katikati Juma Said Makapu pamoja na Paschal Wawa. Ingekuwa ni rahisi sana kwa mabeki hawa kufanikiwa kucheza mipira ya juu pindi wakutanapo na Tp Mazembe au Raja Casablanca.

LihatTutupKomentar