KOCHA MPYA T-STARS NI BALAA

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema lipo katika hatua za mwisho za kumleta Kocha mpya wa Taifa Stars ambaye atawasili wakati wowote kuanzia sasa ili aanze kibarua cha kuinoa timu hiyo

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Wilfred Kidao, ameeleza kuwa Kocha huyo tayari ameshaanza kazi ya kuwafuatilia wachezaji kwa njia ya mtandao ili kupata urahisi wa kuja kufanya kazi vizuri

Kidao amesema TFF ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha mipango ya kumleta mbadala wa Salum Mayanga huku akishindwa kuweka jina lake hadharani kwa madai ya kuwa muda mwafaka haujafika

Katibu huyo amefunguka na kueleza tayari Kocha huyo ameshaanza kuwafuatilia vema kupitia njia ya mtandao wachezaji ambao walikuwa ndani ya kikosi cha Mayanga hivi karibuni. 

Kocha huyo mpya anakuja kuchukua nafasi ya Mayanga ambaye aliiongoza Stars katika mechi kadhaa za kirafiki huku akikumbukwa kwa kuimaliza DR Congo kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa Machi 28 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mwaka huu.

LihatTutupKomentar