HUKO SIMBA NI MAKOMBE TU.

Huko Simba ni makombe mwanzo mwisho. Inshu yenyewe iko hivi klabu ya Simba maarufu kama mnyama imefanikiwa kutwaa kombe la ngao ya jamii baada ya kuifunga klabu ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa CCM karumba uliopo jijini Mwanza. Klabu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo mabao ya katika pambano hilo yamefungwa na mshambuliaji Meddie Kagere dakika ya 29 pamoja na kiungo Hassan Dilunga ambaye alifunga goli la pili na la ushingdi dakika ya 45 huku goli la Mtibwa Sugar likifungwa na mshambuliaji Kevin Kongwe dakika 33. Simba imetwaa kombe hilo la ngao ya jamii mara nne tangu kuanza kwa kombe hilo mnamo mwaka 2001
LihatTutupKomentar