AZAM FC IMEREJEA KWA KISHINDO

TIMU ya Azam FC ilirejea jana kutoka nchini Uganda ambako iliweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unaotarajiwa kuanza Agosti 22, mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba, Azam itafungua dimba Agosti 23, mwaka huu dhidi ya timu ya Mbeya City katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumza na mkomesportnews , Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd, alisema kambi yao ya nchini Uganda imemsaidia kocha mkuu wa timu hiyo, Hans van der Pluijm kukijua kikosi chake, hivyo wachezaji wataanza ligi wakiwa na nguvu.

“Kambi ilikuwa nzuri na benchi la ufundi limepata kile walichohitaji kutokana na maandalizi waliyofanya pamoja na mechi za kirafiki zilizochezwa, sasa tunajipanga kupambana katika Ligi Kuu,” alisema.

Aidha, aliongeza kuwa kikosi chao kipo fiti na wachezaji wote wameimarika kutokana na kambi waliyoweka nchini Uganda wakiwamo wale wa kimataifa waliosajiliwa.

Hata hivyo, Idd alisisitiza kwamba kikosi chao kimejipanga kufanya vizuri katika Ligi Kuu msimu ujao na kuweka rekodi nzuri zaidi ya msimu uliopita kwani timu hiyo haijafanikiwa kutwaa ubingwa kwa muda mrefu sasa.

LihatTutupKomentar