YANGA NAO WANASAFIRI KUJIANDAA NA LIGI KUU

Mara baada ya mchezo kati ya Yanga na Gor Mahia kombe la shirikisho barani Afrika CAF kumalizika kwa Yanga na Gor Mahia Yanga Inatarajiwa kuingia kambini Rasmi kujiandaa na ligi Kuu na mechi zilizobaki Kimataifa.

Yanga itaondoka leo jioni kwenda mkoani Morogoro kwaajili ya maandalizi hayo ya msimu wa Ligi Kuu na Mechi zilizosalia kimataifa.

Mwalimu wa Yanga Mwinyi Zahera ndiye aliyependekeza kambi hiyo kwani amewahi kuwa na Yanga mkoani Morogoro na ameisifia kambi hiyo kuwa ni nzuri na itawafaa wachezaji wa Yanga

KOCHA ATOA MASHARTI KUELEKEA KAMBI HIYO

Kocha Mwinyi Zahera amefunguka kuwa kuelekea kambi hiyo ya Mkoani Morogoro na kusema kuwa ni lazima viongozi wakubaliane naye kwa  wachezaji wafanye mazoezi mara mbili kwa siku.

Kambi iwe ya Kufanya mazoezi mara mbili kwa siku asubuhi na Jioni ili kuwaweka vizuri wachezaji kuelekea msimu mpya.

LihatTutupKomentar