Klabu ya Manchester United inamtaka kumsajili kwa udi na uvumba beki wa kati wa Leicester City, Harry Maguire. Ni kweli huenda England walifanikiwa kufika hatua ya nusu ya fainali kombe la dunia kupitia mgongo wa Harry Maguire. Ukiachana na inshu ya Harry Maguire kuonesha kiwango cha juu akiwa na England pia kuna matukio mengine matatu ambayo yametokea wakati wa fainali za kombe la dunia pale Russia. 3. MATUMIZI YA VAR Ni moja ya matumizi makubwa ya teknolojia ambayo yametumika katika michuano hii ya kombe la dunia iliyomalizika nchini Russia. Video Assistant Referee (VAR) ni teknolojia ambayo inamsaidiarefa au mwamuzi wa mchezo kuamua magoli ambayo yanaonekana yana utata. Matumizi ya VAR yameamua mabao mengi katika mechi mbalimbali za kombe la dunia. Moja ya mabao ambayo yameamuliwa na teknolojia ya VAR ni bao la kiungo Paulo Pogba ambalo alilifunga dhidi ya Australia katika mechi za awali za hatua ya makundi. 2. MABAO YA KUTOSHA. Michuano ya kombe la dunia iliyomalizika Russia pia ni michuano ambayo imetoa mabao ya kutosha. Mfano mechi dhidi ya Tunisia na Ubelgiji ni mechi moja tu ambayo ilitoa jumla ya magoli 7. Lakini kiufupi ni kwamba michuano hii ya kombe la dunia imetoa jumla ya magoli 165
1. USHINDANI MKUBWA. Nadhani hili ndio moja ya matukio au tukio ambalo wengi walikuwa hawalitazamii kutokea. Hii inatokana na timu kubwa ambazo zilikuwa zinapewa kipaumbele kufanya vizuri kwenye michuano hii kuondolewa mapema. Mfano timu kama Ujerumani, Hispania, ni timu ambazo zilikuwa zinapigiwa upatu kufanya vizuri kwenye michuano hii kwa maana ya kutwaa kombe hilo lakini hazikufanya hivyo. Lakini timu kama Mexico pamoja na Crotia hazikuwa zinapewa nafasi ya kufika hatua ya robo hata nusu fainali. Kwahiyo hali hii ina maanisha ushindani ulikuwa ni mkubwa sana katika michuano hii ya kombe la dunia.