KAZI KAZI! Ndio unavyoweza kuielezea kambi ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, hapa nchini Uganda, kutokana na maandalizi makali wanayofanya ikiwa ni siku ya pili tokea iwasili nchini humo.
Msafara wa Azam FC umetua jana mchana nchini humo na kujichimbia katika Hoteli ya Top Five, iliyopo Ntinda, jijini Kampala, wakiweka kambi ya wiki mbili itakayoambatana na takribani mechi nne hadi tano za kirafiki kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam Agosti 16 mwaka huu