TETESI ZA USAJIRI ULAYA LEO

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry, ambaye yuko katika kikosi cha ukufunzi cha Ubelgiji amekubali kwa maneno kuchukua uoingozi wa klaby ya Aston Villa akichukua mahala pake Steve Bruce. (Daily Star) 

Chelsea inajiandaa kuimarisha dau la £45m kumnunua beki wa Juventus na Itali Daniele Rugani, 23, baada ya ombi la hapo awali la £36m kukataliwa. (Goal) 

Chelsea imekataa ombi la tatu la zaidi ya £55m - kutoka Barcelona kumnunua winga wa Brazil Willian, 29. (Sky Sports) 

Arsenal bado ina hamu ya kumsajili kiungo wakati wa Sevill aliyeshinda kombe la dunia Steven Nzonzi, 29,lakini hawako tayari kuafikia matakwa ya kandarasi ya raia huyo wa Ufaransa ya kumuachilia kwa dau la £35m. (France Football) 

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anapanga kumpiga bei winga wa Ufaransa Anthony Martial, 22, kwa dau la £50m lakini kwa klabu ambayo haichezi ligi ya Uingereza. (Guardian) 

Tottenham ina matumaini ya kujipatia £30m kupitia kumpiga bei mshambuliaji wa Uholanzi Vincent Janssen, 24, pamoja na mshambuliaji wa Uhispania Fernando Llorente, 33. (Evening Standard) 

Newcastle iko katika mazungumzo kumsajili beki wa Deportivo La Coruna na Uswizi Fabian Schar, 26, ambaye ana kandarasi inayomzuia yenye thamani ya £3.5m . (Daily Mail) 

Everton inamtaka beki wa Barcelona Lucas Digne lakini imepunguza hamu yao kwa beki wa kushoto wa Scotland Kieran Tierney. Raia wa Ufaransa Digne, 25, ana thamani ya £22m. (Liverpool Echo). 

Klabu mpya iliopanda katika ligi ya Premia Fullham imewasilisha ombi la kutaka kumnunua mshambuliaji wa Brazil na Real Sociedad Willian Jose, 26 kwa dau la £26m. (Sun) 

Kipa wa Uhispania Fabri, 30, amefanyiwa vipimo vya kimatibabu katika klabu ya Fullham akisubiri uhamisho wake wa dau la £5m kutoka klabu ya Uturuki ya Besiktas. (Sky Sports) 

West Ham na Leicester zote zinamnyatia kiungo wa kati wa Juventus na Itali ,25, Stefano Sturaro. (La Gazzetta dello Sport - in Italian)

LihatTutupKomentar