TETESI ZA USAJIRI LEO ULAYA

Manchester City itamuuza mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling katika kipindi cha miezi 12 ijayo iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 hatokubali masharti mapya ya kandarasi yake . 

Kandarasi ya mechezaji huyo inakamilika mwezi June 2020 lakini City haitakubali kuruhusu mchezaji wake yeyote muhimu kukamilisha kandarasi yake.. (Daily Mirror) 

Lakini Sterling anahofia kwamba fursa yake ya kuandikisha mkataba mpya na mabingwa hao wa ligi ya Uingereza imepungua kufuatia mchezo wake wa kiwango cha chini katika kombe la dunia msimu huu.. (Daily Telegraph) 

Aliyekuwa mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger analengwa na shirikisho la soka nchini Japan kuchukua wadhfa wa mkufunzi mpya wa timu ya taifa. Raia huyo wa Ufaransa amesema kuwa bado ana hamu ya kuendelea na ukufunzi. (Daily Mail) 

Chelsea imemuorodhesha kinda wa miaka 19 kutoka klabu ya AC Milan na kipa wa Itali Gianluigi Donnarumma katika orodha ya wachezaji wanaolengwa iwapo kipa wa Ubelgiji Thibaut Courtois,26, anayenyatiwa na Real Madrid ataondoka Stamford Bridge msimu huu. (London Evening Standard) 

Kipa wa Costa Rica Keylor Navas, 31, atasalia na kupigania nafasi yake ya kwanza katika klabu ya Real hata iwapo klabu hiyo ya Uhispania itamsajili Courtois. (AS) 

Beki wa Juventus na Itali Daniele Rugani, 23, atajiunga na Chelsea katika kandarasi ya miaka mitano yenye thamani ya £77,000 kwa wiki, huku Chelsea ikikubali kuwalipa mabingwa hao wa Itali dau la £44.2m. (London Evening Standard) 

Leicester City imekubali malipo ya £12.5m na Liverpool kumnunua kipa wa Liverpool Dany Ward 25, na itakutana na mchezaji huyo wa Wales katika kipindi cha saa 24 zijazo. 

Ward anatahitajika na mkufunzi wa Leicester Claude Puel ili kumpatia ushindani mkali kipa wa Denmark Kasper Schmeichel. (Daily Telegraph) 

Valencia inajiandaa kumsaini beki wa Manchester United Timothy Fosu-Mensah,20, kwa mkopo kabla ya kumpatia mkataba wa kudumu. (Super Deporte) 

Fulham imeimarisha ombi lao la kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania David Lopez, 28, kutoka dau la £13.41m hadi £17.88m. (El Mundo) 

Mchezaji mpya wa Liverpool na Uswizi Xherdan Shaqiri, 26, hakuonekana katika harakati za kuepuka kushushwa daraja kwa Stoke , kulingana na kiungo wa kati wa klabu hiyo Charlie Adam. (Talksport) 

Swansea City imeanza mazungumzo na kiungo wa kati wa Manchester City kutoka Kosovo Bersant Celina katika mkataba wenye thamani ya £4m. (Daily Mirror) 

Sheffield United imewasilisha ombi lililovunja rekodi la £5m kwa mshambuliaji wa Uingereza Martyn Waghorn ,28, kutoka kwa wapinzani wao ligi ya mabingwa Ipswich Town. (Daily Star) 

Mshambuliaji wa United na Wales Ched Evans, 29, ananyatiwa kwa mkopo na klabu ya Fleetwood Town. (@SUFC_tweets) 

Stoke City wanakaribia kuweka makubaliano ya dau la £10m na Huddersfield Town kwa winga wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26 Tom Ince. (Daily Telegraph) 
LihatTutupKomentar