NGOMA OUT AZAM FC

Donald Ngoma hatokuwepo kwenye kikosi cha Azam ambacho leo Jumamosi kinakwenda nchini Uganda kuweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu. 

Ngoma ambaye alijiunga na Azam kwenye usajili huu mkubwa amepewa mapumziko kutokana na kutoka kwenye majeruhi hivyo ataanza mazoezi mwezi ujao. 

Kwa mujibu wa kocha wa meneja wa timu hiyo, Phillip Alando, amesema wakiwa nchini Uganda, wanatarajiwa kucheza mechi tatu za kirafiki ambazo Kocha Hans van Der Pluijm ameziomba ili kukiweka sawa kikosi chake kabla ya ligi kuanza Agosti 22, mwaka huu. 

Baadhi ya timu watakazocheza nazo ni pamoja na Vipers SC iliyokuwa hapa nchini kwa ajili ya KAGAME, KCCA na Express FC. 

LihatTutupKomentar