TAMBWE "LICHA YA MATATIZO YETU YANAYO TUSUMBUA LAZIMA GOR MAHIA TUMPIGE"

Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameibuka na kusema wanaumizwa na hali inayoendelea katika timu hiyo lakini haiwafanyi washindwe kupigana huku wakiwaomba mashabiki kuwa kitu kimoja kabla ya mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia ya Kenya. 

Yanga inatarajiwa kurudiana na Gor Mahia Jumapili ya wiki katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar baada ya ku­fungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Kenya. 

Kwa mujibu wa mkomesportnews , Tambwe alisema kwa sasa bado wanapita katika kipindi kigumu lakini hawezi kuwafanya washindwe kufanya vizuri katika mchezo huo wa maru­diano huku akiwaomba mashabiki wasichoke kuwasapoti. 

“Tunajua matokeo hayakuwa mazuri kwetu katika mchezo wa kwanza kwa sababu hakuna ambaye alitege­mea tutapoteza tena kwa idadi kubwa ya mabao lakini kwa kuwa wenzetu walitumia mapungufu yetu kupata ma­tokeo. 

“Nadhani huu ni wakati wa kuende­lea kushikamana, mashabiki wetu hawa­paswi kuendelea kukata tamaa japokuwa hatupo katika wakati mzuri kama ilivyokuwa za­mani, hakuna ambaye ana furaha na kinacho­tokea kwa sababu wote tunataka kufikia mafanikio na ukiangalia tunaelekea kwenye ligi kwa nini wakate tamaa,” alisema Tambwe.

LihatTutupKomentar