SERGE PASCHAL WAWA KAPEWA MKATABA MNONO SIMBA

Klabu ya Simba imempa mkataba wa mwaka mmoja beki wake raia wa Ivory Coast, Serge Paschal Wawa ambao ndani yake kuna masharti magumu lakini atakuwa akilipwa shilingi Milioni 10 kwa mwezi mshahara ambao ni mara tano na ule anaolipwa daktari bingwa pale Muhimbili.
Simba wameamua kumpa mkataba mfupi beki huyo ili kumtazama vizuri ila ikiridhika naye itamuongezea mkataba mwingine, kwa mujibu wa chanzo cha taarifa hii ambacho hakina shaka yoyote kinasema beki huyo amesajiliwa kama mchezaji huru.
Wawa ambaye aliwahi kuzichezea Azam Fc na El Merreikh ya Sudan amejiunga na Simba na kujaribiwa katika michuano ya komne la Kagame ambapo Simba ilitinga fainali na kufungwa mabao 2-1 na Azam FC, Simba imempa mkataba wenye masharti magumu mlinzi huyo ambapo kama akishindwa kuonesha kiwango chake basi klabu inaweza kuvunja naye mkataba na kumlipa mshahara wa mwezi mmoja tu ambao ni milioni 10
LihatTutupKomentar