Na MOSES FRANCIS
Mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid Cristian Ronaldo tayari ameshasajiliwa na klabu ya Juventus na maisha yanaendelea. Wakati mamilioni ya watu duniani huenda wanaamini kuwa mshambuliaji huyo ndiye mchezaji bora wa muda wote katika klabu hiyo lakini beki wa pembeni wa timu hiyo Dani Carvajal ameibuka na kukanusha mtazamo huo. Beki huyo ambaye aliwahi kucheza na Ronaldo katika klabu hiyo ya jijini Madrid amesikika akisema kuwa " Raul Gonzalez ndiye mchezaji bora wa muda wote wa Real Madrid ni mchezaji ambaye alishinda kila kitu katika kazi yake ya soka, Ronaldo siyo mchezaji bora wa muda wote wa Real