GOR MAHIA YAIGALAGAZA YANGA 4 BILA

FULL TIME | Gor Mahia FC 4 - 0 Yanga FC (24' J. Tuyisenge, 45' 85' E. Guikan, 65' H. Mwinyi - OG).

Yanga imeshindwa kuuweza mziki wa Gor Mahia FC katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuambulia kichapo cha mabao 4-0.

Mchezo huo uliopigwa jijini Nairobi usiku huu umeshuhudia Gor Mahia wakipachika mabao yao kupitia kwa Jacques Tuyisenge, Ephram Guikan aliyefunga mawili pamoja na Mwinyi haji aliyejifunga.

Ushindi huo wa Gor Mahia unawafanya waendelee kukalia nafasi ya pili katika kundi D wakifikisha jumla ya alama 5 huku MC Alger walio kileleni wakiwa na pointi 7 wakati Rayon Sports ya Rwanda ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 2.

Yanga imekuwa timu ya kwanza ndani ya kundi hilo kuruhusu mabao 9 baada ya kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya MC Algeria kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa huko Algeria.

Kikosi hicho sasa kimejiwekea mazingira magumu zaidi kufuzu kuelekea hatua inayofuata kutokana na matokeo mabovu ambapo katika mechi tatu kilichocheza kimeambulia alama moja pekee.
LihatTutupKomentar