Na:MOSES FRANCIS
+255743243120
Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez huenda hapati usingizi kwa sasa. Kiongozi huyo mwenye jeuri ya fedha anahaha kutafuta mshambuliaji ambaye atakuja kuvaa viatu vya Cristian Ronaldo ambaye tayari ametimkia katika klabu ya Juventus. Sasa inshi iko hivi Klabu ya Real Madrid ambayo imeonekana kutokuwa na matumaini ya kumnasa mshambuliaji kinda Kylian Mbappe ambaye alikuwa anapewa kupaumbele kujiunga na klabu hiyo baada ya kuwa ameonyesha kiwango bora katika michuano ya kombe la dunia iliyomalizika nchini Urusi siku za hivi. Klabu ya Real Madrid kwa sasa imehamishia nguvu zao zote kumsajilimshambuliaji raia wa Urugauay na klabu ya PSG Edson Cavan ambaye anaonekana kuwa mbadala sahihi wa mshambuliaji Cristian Ronaldo ambaye ametimukia katika klabu ya Juventus kwa dau la paund milion 99.2. Edson Cavan anapewa nafasi kubwa ya kujinga na klabu ya Real Madrid kutokana na rekodi yake nzuri ya kufunga magoli kunako katika klabu ya PSG. Cavan mpaka sasa amefanikiwa kucheza mechi 245 na kufunga jumla ya magoli 170.