TETESI ZA USAJIRI ULAYA

Manchester United wanajiandaa kuwasilisha ombi la kutoa £60m kumnunua winga Mbrazil Willian, 29, kutoka kwa klabu ya Chelsea kabla ya msimu ujao kuanza. (Mail)
Klabu ya Italia Napoli inadaiwa kutaka kumchukua kipa mwenye uzoefu mkubwa kutoka Jamhuri ya Czech Petr Cech, 36, kutoka Arsenal kwa mkopo. (Gazzetta dello Sport via Sun)
Crystal Palace nao wamejiunga na Arsenal katika kumnyatia kiungo wa kati wa Arsenal ambaye hajatulia Jack Wilshere. Hii ni baada ya kiungo huyo wa miaka 26 kuambiwa na meneja mpya wa Gunners Unai Emery kwamba hawezi kuhakikishiwa kuwa atakuwa anaanza mechi. (Mirror)

Klabu ya Sevilla ya Uhispania inataka kutoa saini mkataba wa kumchukua kiungo wa kati wa miaka 23 anayechezea Real Madrid Marcos Llorente. (AS)
Hilo huenda likatoa nafasi kwa Arsenal kumchukua Mfaranza anayechezea Sevilla safu ya kati Steven Nzonzi, 29, ambaye amewahi kuichezea Blackburn. (Express)
Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25, amekataa kuingizwa kwenye mjadala kuhusu iwapo atasalia katika klabu hiyo akiwa bado na timu ya Ufaransa katika Kombe la Dunia. (Metro)

Kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 23, lazima aoneshe kwamba amejitoleza na 'yuko tayari kuifia' Manchester United ndipo aweze kukubaliwa kuhamia Old Trafford, kwa mujibu wa beki wa zamani wa Manchester United Patrice Evra. (ITV, via Goal)

Wakala wa Mario Balotelli, Mino Raiola, amesema mchezaji huyo wa miaka 27 kutoka Italia ambaye kwa sasa anachezea Nice anaweza kuunga mkono kuhamia Marseille. (RMC Sport)

Leicester wanakaribia kumsaini kiungo wa kati James Maddison baada ya Norwich kukubali kupokea £24m kumruhusu mchezaji huyo wa miaka 21 kuhama. (Mail)

Uhamisho wa kipa wa Roma Alisson kwenda Real Madrid bado haujathibitishwa na Liverpool na Chelsea bado wana nafasi ya kumchukua mlinda lango huyo wa miaka 25. (Gazzetta dello Sport kupitia Express)

Mshambuliaji wa Liverpool anayechezea timu ya England ya wachezaji wa chini ya miaka 17 Rhian Brewster amekubali kutia saini mkataba wa ska ya kulipwa wa kumuweka Anfield, huku akiendelea kutafutwa na klabu kadha za Ujerumani. (Telegraph)

Mchezaji wa zamani wa Leeds United Eddie Gray anaamini kuteliwa kwa Marcelo Bielsa kuwa mkufunzi mkuu ni hatua nzuri ya klabu hiyo kuelekea njia ifaayo. (Yorkshire Evening Post)
Kiungo wa kati wa Denmark Nicolai Brock-Madsen, 25, ambaye alikaa miezi sita klabu ya Cravocia ya Poland kwa mkopo wa miezi sita anatarajiwa kurejea Birmingham City. (Birmingham Mail)

Manchester United itataka dau la pauni milioni 70 kwa ajili ya Anthony Martial 22, ikiwa mfaransa huyo ataendelea kusisitiza kuondoka Old Trafford. (Star Jumapili). Kutokana na nia ya Spurs, Paris St-Germain na Real Madrid, klabu hiyo ya Old Trafford haitamtoa mchezaji wake kwa chini ya pauni milioni 75. (Sunday Mirror)
Maurizio Sarri ameendelea kujiamini kuwa Chelsea itafikia makubaliano na klabu yake ya zamani Napoli ili aweze kuwa Meneja mpya wa Stamford Bridge.(Observer)
Mshambuliaji Real Madrid Gareth Bale amepata ahueni kwa kuwa meneja wake mpya Julen Lopetegui anaweza kuzungumza kiingereza tofauti na Zinedine Zidane. (Express)
Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere,26 anajiandaa kukihama kikosi hicho baada ya kuambiwa kuwa sio sehemu muhimu ya mipango ya Unai Emery. (Sunday Mirror)
Mchezaji wa zamani wa kimataifa Frank Leboeuf anaamini kiungo N'Golo Kante, 27, ni nyenzo muhimu katika matumaini ya Ufaransa kuchukua kombe kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998. (Standard)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amekiri mlinda mlango wake David De Gea, 27 alifanya ''kosa baya'' katika mechi ya kombe la dunia kati ya Uhispania na Ureno lakini amesema ' jambo zuri ni kuwa atakuwepo kwenye mechi itakayofuata, hataogopa, akijiamini na kuwa tayari kusaidia timu''.(Sunday Times
LihatTutupKomentar