ZIJUE SABABU ZA WACHEZAJI WA YANGA AMBAO HAWAJA SAFIRI NA TIMU

Uongozi wa Yanga umewakingia kifua wachezaji wake Kelvin Yondani 'Vidic', Ibrahim Ajib, Papy Tshishimbi na Mzambia Obrey Chirwa walishindwa kusafiri na timu kwenda nchini Algeria kwa sababu ya matatizo mbalimbali.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema, wachezaji hao hawajasafiri si kukusudia, lakini kwa sababu ya matatizo hayo.

Mkwasa alisema, Yondani na Tshishimbi wao walipata maumivu katika mchezo uliopita dhidi ya Simba, Obrey ana malaria wakati Ajib anamwangalia mke wake anayetarajiwa kujifungua hivi karibuni.

"Kama nilivyosema, Yondani, Tshishimbi na Chirwa wao ni wagonjwa na Ajib amebaki kwa sababu mkewe anakaribia kujifungua,"alisema Mkwasa.

Kikosi cha Yanga kilisafiri na Ndege ya Emirates jana Alhamisi kwenda Algeria wakipitia Dubai tayari kwa
mchezo huo utakaochezwa kesho kutwa Jumapili dhidi ya USM Alger.

Wachezaji wa Yanga waliondoka na timu ni Rostand Youthe, Ramadhan Kabwili, Hassan Kessy, Andrew Vincent, Haji Mwinyi, Gadiel Michael, Pato Ngonyani, Said Makapu, Juma Abdul, Yussuf Mhilu, Mwashiuya Geoffrey, Pius Buswita, Rafael Daud, Yohana Nkomola, Emmanuel Martin, Juma Mahadhi, Abdallah Shaibu 'Ninja', na Said Makapu.

LihatTutupKomentar