NGASSA AWAPA USHAURI YANGA

Mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga, Mrisho Ngassa
amewataka mabingwa hao wasitetereke baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Simba badala yake waongeze nguvu katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Ngassa amesema pamoja na kipigo hicho Yanga inaweza kujipanga vizuri na kufanya vizuri katika mechi zake za ligi pamoja na michuano ya Shirikisho Afrika.
Yanga inatarajia kuondoka nchini Mei 3 kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza hatua ya makundi dhidi ya USM Algiers.

Akizungumzia mchezo huo Ngassa amesema Yanga haikuwa imezidiwa sana na wapinzani wao Simba kama ilivyodhaniwa na wengi na waliweza kuhimili vishindo vya Wekundu hao.
"Nadhani haikuwa mechi mbaya sana kwa Yanga waliweza kuwahimili Simba, kikubwa ni kutokata tamaa katika mechi zijazo wakiweka msisitizo kwenye michuano ya Shirikisho Afrika," alisema Ngassa.

Ngassa kwa sasa anachezea timu ya Ndanda FC ya Mtwara ambayo ipo kwenye mstari wa kushuka daraja msimu huu.

LihatTutupKomentar