Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga amewacharukia Azam TV akiwalaumu kutokutangaza kitendo cha Kelvin Yondani kutemewa mate wakati wa mchezo wa Yanga SC dhidi ya Singida United uliofanyika Uwanja wa Namfua.
Mkemi amehoji iweje Azam TV hawajatilia nguvu kutangaza tukio hilo huku akieleza kuwa wao na Simba baba yao ni mmoja.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mkemi amewauliza Azam TV kuwa Camera zao zilikuwa wapi wakati tukio hilo linafanyika? Ina maana hawakuliona hilo?
"Kujisaidie ajisaidie kuku tu, Haji Manara, TFF na Azam TV hii haikushabikiwa wala hamkuitangaza kwakuwa nyinyi na Simba baba yenu mmoja, Azam TV hii kamera zenu haikuona siyo?" aliandika Mkemi
Kauli hiyo ya Mkemi imekuja kuafuatia tukio la beki Yondani lililo gumzo hivi sasa mitandaoni kumtemea mate mchezaji, Asante Kwasi, katika mchezo dhidi ya watani zao wa jadi Simba uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi Jumapili.