Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amewapiga kijembe 'UTANI' watani zake wa jadi Simba kuhusiana na kambi waliyoweka Morogoro
Mkwasa amesema kuwa inawezekana Simba wameweka kambi Morogoro kutokana na kuyumba kiuchumi.
Mkwasa vilevile ameeleza kuwa yawezekana Simba wameshindwa kwenda Zanzibar kuweka kambi huko kutokana na gharama kuwa kubwa, hivyo nao wamemua kuwa Morogoro.
Kijembe amewapiga Simba zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya mtangange dhidi yao kupigwa Uwanja wa Taifa, Jumapili ya Aprili 29 2018.