MKUDE ATAIKOSA LIPULI FC

Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude, ataukosa mchezo wa Simba dhidi ya Lipuli FC utakaopigwa mjini Iringa Aprili 21 2018, Jumamosi ya wiki hii.
Mkude atakosekana katika mechi hiyo sababu atakuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano ambazo kwa mujibu wa kanuni, mchezaji hukosa mechi moja inayofuatia pindi anapofikisha idadi hiyo ya kadi.
Simba itasafiri kuelekea Iringa wiki hii kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Samora.
Kikosi hicho kitakuwa kinacheza na Lipuli kikiwa na harakati za kuwania ubingwa wa ligi ambao umekosekana Msimbazi kwa takribani miaka mitano.

LihatTutupKomentar