MFUPA WA TUKUYU STARS UNAVYOWATESA TIMU NGENI LIGI KUU TZ.



na Godfrey Mgaya

Joseph Kasyupa na Abdul Lausi Ni miongoni mwa majina ambayo hayatasahaulika katika historia ya soka mkoani mbeya, hususan Wilayani Rungwe kunako mji mdogo wa Tukuyu. Miaka ya 1981 marafiki hawa waliunganisha mawazo yao katika Kuitafuta timu moja ambayo itaiwakilisha tukuyu katika ligi kuu tanzania bara.

Wawili hawa waliamini kwamba tukuyu ina vipaji vingi kisoka hivyo kama wataamua kuunganisha nguvu zao wataweza kuunda timu moja iliyo madhubuti.  Hapo wakaamua kushirikisha watu wazo lao na kupokelewa vema.

Mwishoni mwa 1981 waliweza kuunganisha nguvu ya vilabu viwili nguli Mwenge fc na jamuhuri fc za tukuyu. Viongozi wa vilabu hivi waliunga mkono wazo la kujumuisha nguvu zao katika kuunda timu moja.

Mwaka 1982 Mkutano wa kwanza ulifanyika tukuyu. Na mdhamini alipatikana baada ya harakati za viongozi wa timu hiyo. na mdhamini mkuu alikua mfanya biashara mashuhuri rungwe Pater Kaka huyu ana asili ya kihindi. katika kikao hiko Walipitisha jina la Limbe leaf kama jina la timu, Baraza la michezo BMT ilikataa kusajili jina hilo kwasababu tayari linatumika huko Malawi kuna timu ilikua ikiitwa hivyo.

Mke wa Mdhamini mkuu pater kaka akapitisha jina la Tukuyu stars na wajumbe wa kikao wakapitisha jina hilo. wao wakaongezea Banyambala  ikimaanisha (wanaume). Baada ya hapo tukuyu ilianza harakati zake za kupanda madaraja.

Mwaka 1986 ilifanikiwa kupanda daraja na kushiriki ligi daraja la kwanza  (sasa ligi kuu tanzania bara). Tukuyu stars ilikua na kikosi cha dhahabu ambacho kiliundwa na mashujaa Wengi wakiwemo Betwell Afrika, Sekilojo Chambua, Chachala Muya, Asanga Aswile, Mbwana makata, Daniel Chundu na wengine wengi.

Tukuyu stars banyambala Waliandika rekodi kubwa ambayo ni ngumu kuvunjwa. Rekodi ya kuchukua Ubingwa wa ligi daraja la kwanza katika msimu wake wa kwanza. Rekodi hizi huwenda zikawa chache zaidi Katika maisha yote ya soka.

Tukuyu stars baada ya kubeba taji la ushindi Misimu michache baadae ikashuka daraja na kurudi ligi daraja la pili. na hii ilitokana na wachezaji wake wengi nguli kuchukuliwa na vilabu vikongwe.

Alichokifanya tukuyu tunasubiri kukiona kwa mbwana Makata ambaye alikua katika kikosi cha tukuyu mwaka 1986, kwa sasa ni mwalimu wa Alliance ya mwanza aliyopanda daraja msimu huu kwenda ligi kuu. Je mbwana makata ataweza kutumia mbinu na maarifa ya tukuyu stars Kurudia rekodi aliyoiweka Miaka ya 1986?

KMC, African lyon, Biashara Mara, Jkt Tanzania, Coastal union, na Alliance ni timu zilizopanda ligi kuu msimu ujao 2018/2019 nani ataweza kuula mfupa wa Tukuyu stars Ambao umeshindikana kwa Singida united, Njombe mji na Lipuli? katika msimu uliopita?

Tusubiri kuona. Tukuyu ilitokea kuzimu ikapotea kusikojulikana.
LihatTutupKomentar