Kocha Mpya wa Yanga, Zahera Mwinyi leo anakutana na wachezaji pamoja na viongoiz wengine wa benchi la Ufundi mkoani Morogoro.
Zahera yuko mkoani Morogoro kwa ajili ya jukumu hilo kisha atarejea jijini Dar es salaam kukamilisha taratibu za kiofisi kumuwezesha kufanya kazi nchini.
Jana Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alifanya mazungumzo na kocha huyo.
"Tumemruhusu kwenda kukutana na timu, apate kujua baadhi ya mambo muhimu kutoka kwa vijana na viongozi wengine wa benchi la ufundi, baada ya hapo atarejea Dar kuja kukamilisha taratibu za kuanza majukumu ikiwa ni pamoja na mambo ya mikataba.
"Binafsi nafahamu ni kocha mzuri amekuwa na mafanikio kwenye timu nyingi alizofundisha na pia anafanya kazi na makocha wakubwa hivyo tunaamini uzoefu alionao unakuja kuleta changamoto mpya kwenya kikosi chetu," Mkwasa ameiambia tovuti ya Yanga
Yanga iko mkoani Morogoro ikiendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Simba April 29 pia mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger May 04.
Yanga inatarajiwa kusafiri kwenda nchini Algeria baada ya mchezo wa Jumapili dhidi ya SImba