Na g̾ o̾ d̾ f̾ r̾ e̾ y̾ ̾ m̾ g̾ a̾ y̾ a̾ ̾
10. Eliund Ambokile – Mbeya City
Moja ya washambuliaji chipukizi wanaofanya vizuri akiwa na kikosi cha MbeyaCity huku akiwafukuzia mastar wakubwa katika ufungaji bora. Mpaka sasa amefunga magoli 10 katika VPL na kuisaidia kwa kiasi kikubwa timu ya Jiji kua katika nafasi za katikati katika msimamo wa ligi.
Katikausajili wa dirisha dogo alitajwa kuwaniwa na YangaSc lakini haikua hivyo, lakini kwenye usajili ujao huenda lolotee likatokea kwa chipukizi huyu.
9. John Mbise – Mshikamano FC
kiungo huyu ameitumikia timu ya daraja la kwanza Mshikamano akitokea Dodomafc katika raundi ya kwanza. Takwimu zake zinavutia kidogo katika daraja alilopo, akiwa katika timu ya Dodomafc chini ya Julio alifanikiwa kucheza michezo mitano huku akitoa assist 2 katika raundi ya kwanza, akiwa na Mshikamano katika raundi ya pili alifanikiwa kucheza mechi nne huku akifunga mara mbili na kuassist mara mbili na kuisaidia timu hiyo kumaliza nafasi nzuri baada ya kuikuta ikiwa mkiani na kuinusuru isishuke daraja.
Kwa takwimu hizo kwa mchezaji wa eneo la kiungo huenda viwakawatoa udenda timu mbalimbali za VPL huku klabu ya African Lyon iliyopanda daraja ikitajwa kumfukuzia mchezaji huyo.
8. Ally Ahmed Shiboli – JKT Tanzania
Mshambuliaji wa zamani wa Coastal Union na SimbaSc amerudisha makali yake ya ufungaji katika kikosi cha JKT Tanzania na kuisaidia kurudi ligi kuu na kuipeleka nusu fainali ya Azamsports FederationCup ambapo alifunga goli moja katika robo fainali dhidi ya Tanzania Prisons Mbeya. Pia alifanikiwa kufunga mabao mawili ya kuamua kupanda ligi kuu katika mechi ya JKT Tanzania dhidi ya Mshikamano iliyopigwa katika uwanja wa Mbweni JKT.
Kwa moto huu huenda vilabu mbalimbali vya VPL vikavutiwa nae kutokana na uzoefu wake wa kucheza Ligi Kuu Bara.
7. Adam Salamba – Lipuli fc
Alianza msimu huu akiwa na kikosi cha Stand UTD kabla ya Matola kumchukua katika kikosi chake chá Lipuli. Tangu mzunguko wa pili umeanza ameonyesha kua ni moto wa kuotea mbali huku akifunga magoli muhimu ya Lipuli.
Katiya magoli mazuri aliyoyafunga ni pamoja na lile alilowafunga Ndanda FC na lile alilowafunga SimbaSc.
6. Habibu Kyombo – Mbao fc
Anajulikana kama kiboko ya vigogo hii ni baada ya kuzitungua timu mbili vigogo za SimbaSc na Yanga tena magoli safi kabisa.
Mpakasasa ana magoli 9 ya ligi huku pia akiwahi kufunga magoli 5 katika mechi moja katika michuano ya Azamsports FederationCup.
5. Marcel Kaheza – Majimaji FC
Kwa sasa ndie askari anaeongoza vitani katika mapambano ya kuisaidia Majimaji isishuke daraja, huku akiwa ameweka kambani magoli 10 mpaka sasa.
Licha ya kucheza kama mshambuliaji wa kati lakini pia ana uwezo wa kucheza nafasi zote za ushambilliaji. Pia ni mzuri katika upigaji wa mipira iliyokufa na kuzidi kuipa faida ya magoli timu yake.
4. Ditram Nchimbi – Njombe Mji
Alianza kuonekana katika soka akiwa na Majimaji FC kisha MbeyaCity na msimu huu kujiunga na Njombe Mji. Kwa kiasi kikubwa amesaidia kuongeza uzoefu katika safu ya ushambilliaji kwenye timu huku akiiongoza katika mapambano ya kuiepusha timu isishuke daraja. Inasemekana ndie mchezaji ghali zaidi katika kikosi cha Njombe Mji cha msimu huu.
3. Ally Ally – Stand UTD
Beki huyu kutoka Zanzibar ameweza kujipambanua na kuonyesha yeye sio mtu wa mchezo mchezo kwenye VPL.
Amekuamchezaji muhimu katika timu yake ya Stand katika safu ya ulinzi wa timu hiyo
2. Hassan Dilunga – Mtibwa Sugar
Unaweza kusema amerudi katika ubora wake, baada ya kutoka Yanga. Alipitia katika vilabu vya Stand UTD, JKT Ruvu na sasa Mtibwa Sugar ambako anaonekana amerudi katika ubora wake huku akiwa ameifungia magoli muhimu timu yake ya Mtibwa. Huwezi kutaja mafanikio ya Mtibwa mwaka huu haswa katika kombe la FA bila kumtaja Hassan Dilunga.
1.Mohamed Issa “Mo banka” – Mtibwa Sugar .
Kiungo huyu wa Mtibwa ameweza kuingia katika timu ya Mtibwa Sugar na kukihakikishia nafasi ya kuanza moja kwa moja. Lakini pia amekua hakosekani katika kikosi cha Timu Ya Taifa kila mara kutokana na uwezo wake mkubwa. Hii imemfanya kujiweka sokoni.