BODI YA LIGI WAPOKEA MALALAMIKO YA YANGA

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekiri kupokea rufaa ya Yanga yenye malalamiko mbalimbali ikiwemo suala la wachezaji wa Mbeya City kuzidi Uwanjani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, amethibitisha kupokea rufaa hiyo ambaye imewasili ndani ya muda mwafaka.
Wambura ameeleza kuwa wameishaipokea na sasa kitakachofuata ni kupelekwa ndani ya Kamati ya Masaa 72 kujadiliwa kisha watatoa mrejesho.
Yanga waliwasilisha rufaa yao ambayo tayari imeshalipiwa ikiwa ni saa kadhaa baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City kumalizika kwa sare ya 1-1 katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.


LihatTutupKomentar