YASEMAVYO MAGAZETI YA BARANI ULAYA LEO JULAI 11, 2017


Chelsea wanajaribu kumnasa Pierre Emerick
Aubameyang,Mara Baada ya kumkosa Romelu
Lukaku.(daily express )
Arsenal wamewasilisha ofa kwa klabu ya
Eintracht Frankfurt wakimwitaji Aymen
Barkok.(daily star )
Alexis Sanchez anajiandaa na msimu mpya
akiwa na Arsenal , kwani klabu hiyo haina
mpango wa kufikiria ofa kutoka Manchester
City ambayo ni chini ya Pauni milioni 90 kwa
ajili ya mchezaji Huyo raia wa Chile.(the
independent )
Mlinda mlango wa Manchester City Joe Hart
atakosa safari ya klabu hiyo ambayo itaenda
marekani zikiwa ni juhudi za mchezaji Huyo
kuondoka klabuni hapo.(daily mail)
Winga wa klabu ya Leicester City Demarai
Gray amepewa ahadi ya kupewa muda mwingi
zaidi wa kucheza na kocha wa klabu hiyo
Craig Shakespeare(daily Mail).
Jose Mourinho anataka mtendaji mkuu wa
klabu ya Manchester United Ed Woodward
kupeleka ofa isiyopingika ya Pauni milioni 60
kwa mahasimu wao klabu ya Tottenham
kumnasa Eric Dier.(daily Mirror ).
Arsene Wenger anaamini kuwa Alex Oxlade-
Chamberlain atabaki Arsenal majira haya ya
kiangazi.( daily mirror )
Mchezaji wa West Ham United Sofiane
Feghouli uenda akatimukia katika klabu ya
Galatasaray kwa uhamisho wa ada ya pauni
Milioni 4.5 baada ya kucheza msimu mmoja
kwa wagonga nyundo hao.(The sun)
Arsene Wenger hatamuuza Olivier Giroud
mpaka pale itakapokuwa wazi kama Alexis
Sanchez atabakia klabuni hapo, Au kama
Monaco wataamua kumuuza Thomas Lemar.
(the daily telegraph )
Celtic wanampango wa kukamilisha dili la
kumsajili kiungo Olivier Ntacham kutoka
Manchester City kwa dau la pauni milioni 4.
(daily record).


LihatTutupKomentar