WENGER – ‘KILA MTU ANAMTAKA MBAPPE, SANCHEZ HATAKI KUONDOKA ARSENAL!’


Akiongea huko Sydney, Australia, ambako Arsenal wako Ziarani kwa matayarisho ya Msimu Mpya, Meneja wao Arsene Wenger amekiri kuwa Staa wa Miaka 18 wa AS Monaco, Kylian Mbappe, anatakiwa na kila Timu wakiwamo wao huku pia akipinga Ripoti zilizozagaa kuwa Staa wao kutoka Chile, Alexis Sanchez, anataka kuihama Klabu hiyo.

Kuhusu Mbappe, Wenger ameeleza: “Ni Mchezaji anaeweza kuamka Asubuhi yeyote na kuamua popote anapotaka kwenda. Si Wachezaji wengi wenye bahati hiyo na yeye ana Miaka 18 tu na lipo Zulia Jekundu mbele yake!”

Alipoulizwa kama Arsenal nao wanamtaka Mbappe, Wenger alijibu: “Sidhani kama kuna Mtu atasema hamtaki Mbappe!”

Mbappe ndie alietoa mchango mkubwa kwa As Monaco kutwaa Ubingwa wa Ligi 1 huko France kwa Msimu wa 2016/17.

Wakati huo huo, Wenger amezipinga Ripoti kuwa Fowadi wao Alexis Sanchez anataka kuihama Arsenal.

Hivi sasa Sanchez, ambae bado hajajiunga na Kikosi cha Arsenal kwa vile Vakesheni yake imeongezwa kutokana na ushiriki wake wa FIFA Kombe la Mabara, anahusishwa sana na kuhamia Manchester City na Bayern Munich.

Sanchez, ambae yupo Arsenal kwa Misimu Mitatu sasa na Msimu uliopita kupiga Bao 24 za Ligi, ndio anaingia Mwaka wa Mwisho wa Mkataba wake na Arsenal na hadi sasa amegoma kusaini Mkataba Mpya.

Wenger amedai kuwa Mwaka wa Mwisho wa Mkataba hakumaanishi kuwa Mchezaji ataihama Klabu kwani anaweza kuongeza Mkataba Mpya.

ARSENAL – ZIARANI-Mechi kabla Msimu Mpya kuanza:

13 Julai v Sydney FC, ANZ Stadium, Sydney

15 Julai v Western Sydney Wanderers, ANZ Stadium, Sydney

19 Julai v Bayern Munich (Shanghai Stadium) International Champions Cup

22 Julai v Chelsea (Bird’s Nest Stadium, Beijing)

29 Julai v Benfica, Emirates Stadium (Emirates Cup)

30 Julai v Sevilla, Emirates Stadium (Emirates Cup)

6 Agosti v Chelsea, Wembley Stadium (Community Shield)

Magical Place

LihatTutupKomentar