TETESI ZA USAJILI ULAYA LEO JULY 03. 2017



Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amgeukia mshambuliaji wa Leicester City, Riyad Mahrez baada ya Monaco kuonekana kuwa wagumu kumuachia Thomas Lemar.

Chelsea na Juventus zimeingia katika vita nyingine ya uhamisho ya kumwania beki wa kulia wa Real Madrid, Danilo.

West Ham imevaa Liverpool katika vita ya kuwania saini ya mshambuliaji wa Benfica, Raul Jimenez.

Nahodha wa zamani wa Chelsea, John Terry yupo mbioni kusaini mkataba wa kuichezea Aston Villa katika dili la mshahara wa pauni 60,000 kwa wiki.


Alexandre Lacazette

Rais wa klabu ya Lyon, Jean-Michel Aula amesema dili la mshambuliaji Alexandre Lacazette litakamilika ndani ya siku moja au mbili zijazo.
LihatTutupKomentar